KIINGEREZA  I  KISWAHILI
KAMPUNI YA UNGA WA NGANO WA AZANIA YASAIDIA MICHEZO
KAMPUNI ya Ngano Azania imekabidhi jezi seti nne kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC), Baraza la Wawakilishi, Tanzania Stars na timu ya Zanzibar Veterani kwa madhumuni ya kutumika katika mechi maalum za kusheherekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jezi hizo zilikabidhiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Adhania, Bw. Awadh Fuad na Meneja Masoko wa Kampuni ya Ngano ya Azania, Mohamed Bashrahil katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Hadees.

Bashrahil alisema kuwa sababu kubwa ya kutoa msaada huo ni kutambua umuhimu wa maendeleo ya michezo nchini na vile vile kama sehemu yao ya kutambua Muungano wa Tanzania na hasa Sikukuu ya Mapinduzi.

Habari Zaidi>>
 
Copyright © MIKOANI TRADERS LTD. All rights reserved.
Designed & Maintained by DESIGN ZONE